Afisa wa polisi akisimamia mizigo ya abiria waliokuwa wakisafiri katika basi la SB lenye namba za usajili T607 BDG lililokuwa njiani kuelekea Dar es salaam kutoka Nachingwea na kupata ajali katika kijiji cha Mchinga mkoani Lindi. Abiria 21 wamejeruhiwa na wamelazwa kwa matibabu katika hospitali ya mkoa Lindi.
Basi la SB lenye namba za usajili T607 BDG lililokuwa njiani kuelekea Dar es salaam kutoka Nachingwea baada ya kupata ajali katika kijiji cha Mchinga mkoani Lindi. Chanzo cha ajali hiyo bado kujulikana
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akiwafariji majeruhi wa ajali hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akimwangalia mmoja wa watoto ambao ni majeruhi wa ajali hiyo. Picha na Abdulaziz Video
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...