Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi za Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat (wapili kulia) wakati Mkuu huyo pamoja na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya kamati hiyo na Wizara. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Kushoto ni Profesa Umesh Kadam, Mwanasheria ICRC katika kanda hiyo na Martha Kassele, Ofisa wa Program ICRC. 
Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi za Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya kamati hiyo na Wizara. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimshukuru Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi ya Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat kwa kumtembelea ofisini kwake na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na ICRC. Kulia aliyekaa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Kushoto ni Profesa Umesh Kadam, Mwanasheria ICRC katika kanda hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...