Waziri wa Ujenzi Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amefungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari katika mji wa Dodoma.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng.Musa Ibrahim Iyombe Mradi huo ambao umefanywa na wakandarasi Wazawa umegarimu shilingi Milioni 384.Mataa yaliyozinduliwa leo ni yaliyopo ANJIA PANDA ya Barabara ya Nyerere na Mpwapwa na yale yaliyopo njia panda ya Barabara ya Area D na barabara  ya kuelekea Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Dkt.Rehema Nchimbi kulia akimkaribisha  Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli Kufungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
 WAZIRI WA UJENZI DKT.JOHN MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MANYONI MJINI YENYE UREFU WA KILOMITA NNE

 WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIWA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA SINGIDA DKT.PARASEKO KONE, MBUNGE WA MANYONI JOHN CHILIGATI PAMOJA NA MWENYEKITI WA WENYEVITI WA CCM MGANA MSINDAI WAKIFUNGUA JIWE LA MSINGI KUASHIRIA UJENZI WA BARABARA HIYO. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2014

    Wizara ya ujenzi imefanya vizuri kuwapatia fursa ya kujenga taa za barabarani wakandarasi wazawa. Wapatiwe fursa zaidi ili ajira ziongezeke na faida ibaki na kuwekezwa humu humu nchini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...