Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa
Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa
sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata
simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa
mienzi mitatu kuanzia leo.
Afisa Mauzo wa airtel Nizar Aladawy na Afisa Mauzo wa Techno bi, Lolinda Joshman wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo. Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo.
Airtel kupitia huduma ya Switch on yazindua ofa kambabe ya simu ya Tecno H5
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Switch on
leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata
simu ya kisasa ya TECNO H5 pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu
kwa muda wa mienzi mitatu.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo
alisema" ofa hii maalumu itawawezesha wateja kununua simu hii ya TECNO
H5 na kupata simcard ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha muda
wa mienzi mitatu kitakachomuwezesha kupiga simu katika muda huu wa
mienzi mitatu kwa gharama nafuu ya shillingi 1 kwa sekunde".
"TECNO H5 ina vitu vinavyovutia ndani ya simu kama vile , camera aina
ya Mega pixel yenye uwezo wa kutoa picha nzuri, nafasi ya kutunza data
wa kiasi cha 4GB, pamoja na memory card yenye ukubwa wa mpaka 32GB,
simu hii pia inatumia technologia ya android na pia ni raisi kuibaba
kwani ina ukubwa wa kati.
Simu ya TECNO H5 inapatikana katika maduka yote Tanzania kwa kiasi cha
gharama ya shilingi 129,000/= "aliongeza Tembo.
TECNO H5 itawapa nafasi wateja wa Airtel kupata huduma ya internet na
kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON iliyowekwa maasusi kwa watumiaji
wa huduma ya internet Tanzania, na kuwapatia internet ya kasi kwa bei
nafuu. Kupata huduma hii ya SWITCH ON ni rahisi mteja anatakiwa kupiga
*148*22# na kuchagua kifurushi cha internet na kisha kupata ujumbe
utakao muhakikishia kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON na kuanza
kufurahia intenet bila kikomo.
Ofa hii ni kati ya ofa nyingi zinazotolewa na Airtel kwa wateja wake,
sambamba na ofa hii ya TECNO H5 Airtel pia inatoa vifurushi vya
YATOSHA vya kupiga simu,ujumbe mfupi , internet na pamoja na ofay a
HAKATWI MTU HAPA inayowawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa kwa
nusu gharama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...