MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera Bi. Zipora Pangani
ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel kwa kufungua duka kubwa,
ambalo litatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kutuma na kutoa
fedha ya (AIRTEL MONEY).
Akifungua duka hilo lililopo eneo la Mtaa wa Kawawa Mjini Bukoba,
alisema litakuwani chachu ya maendeleo, kwa wakazi wa mkoani Kagera
ambapo litarahisisha huduma kwa wananachi.
“Ufunguzi wa hili duka hapa kwetu litakuwa ni chachu ya maendeleo
kwa wateja wa Air tel na wananchi kwa ujumla hasa kwenye matumizi ya
huu mfumo wa air tell money” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa kagera na maeneo jirani
kuhakikisha kwamba wanaitumia hiyo fursa vizuri ili kuhakikisha
wanakuza uchumi wao katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania alisema
ufunguzi wa duka hilo ni mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine nchi
nzima ili kutoa huduma bora kwa wateja wake.
“ Kampuni yetu ya Airtel tuna mpango madhubuti wakuhakikisha maduka
yetu yote yanakuwa na mwonekano sawa na kutoa huduma bora zenye
kiwango cha hali ya juu kwa wateja wetu kutokana na mahitaji yao”
Aliongeza
“ Dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendeana na kasi ya uhutaji kwa
wateja wetu kwenye mawasiliano ya kisasa na teknolojia, ya hali ya
juu” Alisema Mkurugenzi huyo.
Kwa Upande wao wateja wa kampuni hiyo waliojitambulisha kwa majina ya
Joseph Kamuntu na Eradius Ernest wakizungumza mara baada ya
kufunguliwa kwa duka hilo waliishikuru kampuni hiyo na kwa kuwasogezea
huduma hiyo.
“ Tunawashukuru sana hawa watu jamani yaani binafsi nimefurahi sana
kupata hii huduma karibu sasa hivi wamefungua nimeingia mara moja
nimehudumiwa ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine,” Alisema
Kamuntu.
Aliyaomba Mkampuni mengine ya simu kuiga mfano wa kampuni ya Airtel
kwa kutoa huduma bora ambazo zinamjali mteja ili kuhakikisha maendeleo
yanakuwa kwa pande zote.
Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel hadi sasa imefungua maduka 11 hapa
nchini katika mikoa ya Dar es salaam, Kagera, Dodoma ,Morogoro,
Mtwara, Mbeya, lengo likiw ani kuhakikisha wananachi wanapata huduma
bora na kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akikata utepe kuashiria
ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, anaefuata ni
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) na
watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo
litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera ..jpg)
.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akiongea na wananchi na wanahabari waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) pamoja na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (kushoto) akimuelezwa jambo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani mara baada ya ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani (kati) akikata keki
maalum iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja Bukoba
kwaajili ya hafla ya kusheherekea ufunguzi wa duka jipya la Airtel
mkoani hapo. Wakwanza kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi wa huduma kwa
wateja wa Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba na meneja wa duka hilo
bukoba bi Anna Mapunda, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa
Kagera .
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...