Gari aina ya Nissan Hard Body yenye Namba za Usajili T 524 ALW likiwa limetupwa mtaroni na trela la lori (halipo pichani) ambalo lililigonga gari hilo na kutumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach Mchana wa leo. Katika Ajali hiyo iliyohusisha Lori na gari aina ya Nissan Hard Body hakuna mtu yoyote aliyepoteza Maisha
 Wananchi wakisaidia Kulifunga minyororo gari aina ya Nissan Hard Body ambayo imetumbukia mtaroni mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo katika Eneo la Mbezi Afrikana

Wananchi wakisaidia kuligeuza gari ndogo aina ya Nissan Hard Body iliyotumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo, katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...