Marehemu Bi Aziza enzi za uhai wake.
Kikundi cha Unity Of
Women Friends,Kupitia mradi wao wa Mwanamakuka Awards na Washirika
wake,Benki ya Wanawake TWB na Clouds Media Group,Wana tangaza kwa masikitiko makubwa
ya kumpoteza mshindi wa mwaka jana 2013,Bi Aziza Mbogolume (pichani).
Bi
Aziza amefarika mapema jana mchana jijini Dar es salaam,mazishi yake
yanatarajiwa kufanyika leo mnamo majira ya saa 9,na msiba upo nyumbani
kwake Magomeni mwembechai.Aziza alikuwa ni Mwanamke jasiri mwenye
uthubutu wa kufanya biashara kupitia kipaji chake cha Kuchora .
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN
![]() | |
Aziza Mbogolume (wa pili kulia) enzi za uhai wake wakati akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya Mwanamakuka 2013 kutoka kwa Mke wa Makamu wa Rais, Aisha Bilal. |
Baadhi ya viongozi waratibu wa shindano la Tuzo za Mwanakuka wakistaajabia kazi za mikono ya Aziza Mbogolume (wa pili toka kushoto) enzi za uhai wake katika maonesho ya mwaka huu yaliyofanyika Escape 1 Mikocheni jijini Dar |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...