Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika visiwa vya Comoro, amefanya mazungumzo na Bw. Yogesh Manek, Mwenyekiti wa Bodi ya Exim Bank, kwenye Makazi ya Balozi, mjini Moroni. Maudhui ya mazungumzo hayo yalihusu azma ya Ubalozi ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Comoro kwa lengo la kuwezesha kila upande kutambua wafanyabiasha wanaotambulika na kuaminika na pia kuwahamasisha kufanya baishara kwa kutumia taratibu rasmi. Uongozi wa Exim Bank umekubali kusaidia kifanyanikisha azma hiyo.
Mhe. Balozi na Bw. Manek walizungumzia pia uwezekano wa Exim Bank kudhamini mradi mkubwa wa umeme ambao unategemewa kuanzishwa kati ya Shirika la Umeme la Comoro na Kampuni ya DACC Global ya Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya NSI Energy ya Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...