
Mwenyekiti UVCCM mkoa
wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi
wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano
huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM
Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi
mabaya ya fedha za umoja huo.

Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally
Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu
Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za
UVCCM mkoa wa Arusha.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM
Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi (katikati) pamoja na wajumbe wenzake
wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa
ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji
lie linaangalia watendaji wenye sifa.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatulia
maazimio yaliyofikiwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha
kilichofanyika leo jioni.Ambapo Baraza hilo liliazimia kuanza kufanyiak
kwa ukaguzi wa mara kwa mara katika ofisi za UVCCM mkoa kwa kila mwezi
kwa ajili ya kdhibiti ubadhilifu.


Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la
UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia maazimio yaliyokuwa yakisomwa mbele ya
wanahabari leo mjini hapa ambapo Baraza hili liliazimia kwamba endao
Katibu wa Mkoa Mary Chatanda atabainika kuwa na ubadhilifu basi
asihamishwe mkoa mwingine na apelekwe mahakamani ili iwe
fundisho.
picha kwa hisani ya woindeshizza blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...