Mkuu wa Morogoro Joel Bendera akipiga mpira
kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akikagua timu wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.
Bendera atilia mkazo soka la vijana.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera, atilia mkazo
soka la vijana na kuwataka viongozi wa mpira wa miguu mkoa wa Morogoro na chama
cha mpira wa miguu Tanzania kutilia mkazo program za vijana.
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa – Taifa Stars atoa
changamoto wakati akifungua mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro siku ya jumanne. Alisema kuwa hakuna njia
ya mkato katika maendeleo ya mpira wa miguu zaidi ya kuwekeza katika shule za
soka na programu za vijana kama Airtel Rising Stars. Awapongeza Airtel kwa mchango wao.
Zaidi ya majuma mawili kumekua na maoni ya kutoka
kwa wakuu wa mikoa na wadau wengine wakisisitiza viongozi wa mpira wa miguu
nchini kutilia mkazo programu za vijana kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri.
Wakifungua mashindano ya Airtel Rising Stars katika
mikoa yao hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Said Meck Sadiki na Mkuu
wa mkoa Mbeya Abbas Kandoro nao walitilia mkazo kuwekeza katika mpira wa
vijana. Wengine waliotoa maoni hayo ni meya wa Mwanza Stanslaus Mabula na
Mbunge wa Ukonga Eugen Mwaiposa.
Mashindano ya Airtel Rising Stars yanaitimishwa leo
(August 7) na timu zinatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-Salaam siku ya jumamosi
August 9 katika fainali za taifa ambazo zinaanza kutimua vumbi jumapili katika
kiwanja cha kumbukumbu ya Karume. Fainali za Taifa zitamalizika tarehe 17 August na
wachezaji wakiume na wa kike watakao chaguliwa wataweka kambi jijini
Dar-es-Salaam wakijiandaa na mashindano ya kimataifa Airtel Rising Stars
yatakayofanyika nchini Gabon.
Mwaka jana mashindano hayo yalifanyika nchini
Nigeria na timu ya wasichana ya Tanzania walinyakua ubingwa na kuzawadiwa
dollar za marekani 10,000.
Hahahaha isipokuwa Kiongozi Mkuu wa Mkoa Joel Bendera mmemvalisha ngozi ya chui kwa Fulana ya Airtel (Nyekundu) Msimbazi wakati yeye ni Yanga!
ReplyDeleteHuyu alipelekwa kusomea kandanda ujerumani ya Magharibi ili aje kunyanyua soka la bongo. Alikochi timu ya taifa kidogo alivyorudi ila naona hela ipo kwenye siasa. Kila mtu mwanasiasa.
ReplyDelete