Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii 


 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.


Kadhalika, Ekelege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.

“Kwa upande wa  shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi” alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.

 “Mahakama inamuona mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.

“Katika ushahidi uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu Mmbando.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Pole sana mzee na familia kwa ujumla. Kama nikweli ulitumia madaraka vibaya itabidi uwajibike.Hukumu ya uhujumu uchumi ilikuwa ni miaka saba sasa naona wamerekebisharekebisha au ndio basi umetolewa kafara tu.
    mwendo huo uendelee na kwa vigogo wengine pia.

    ReplyDelete
  2. Sijui nianze kuamini.....kua wale wote walioisababishia serikali hasara kwa kuruhusu misamaha wakati wa kuwahukumu kwa makosa yao ndio umefika maana lawama za aina hii zimetokea ktk sehemu nyingi nyeti au labda ni ........sijui simba wa kafara????+++++

    ReplyDelete
  3. Japo nasikitika kuwa mzazi/kaka/Baba wa mtu amekutwa na hatia na anaadhibiwa naona ni sawa sawa tu. Sasa Uncle Michuzi tafadhali uendelee kuandika habari kama hizii. Kwa maana kila kukicha tunapata ripoti, kakamatwa mtu na madwa, mara wengine wanaua, mara ma Albino wameumizwa, halafu basi. Labda wimbi jipya la habari linakuja...naona mahakimu wanaanza kuamka....au ndiyo mushtuo tu..... Haya yetu macho na masikio.

    ReplyDelete
  4. Daa!, Maskini, namjua huyu Mzee, he gave us a training on ISO 2001:9000 standards, too bad he has to go to prison.

    ReplyDelete
  5. samaki wadogo huliwa na mkubwa ndio sheria ya ya baharini iliyowekwa na mungu mwenyewe tangu Enzi sasa kosa la muheshimiwa huyu ni kuwa samaki mdogo wale wote walio wakubwa si rahisi kuliwa na wadogo,labda nikumbushe tu sharia hii waziri wa fedha marehemu kighoma malima alisamehe ushuru wa mamillioni kama si mabillioni kwa baadhi ya wafanya biashara wakubwa kwa amri au barua kutoka ikulu kwa rais mwinyi nani mumemuona alikwenda jela?
    mara nyingi mwizi wa Nazi au embe huenda jela na yule anayeiba nyumba husamehewa kwa wale walnaoshangaa nyumba kuibiwa msishangae huibiwa na utaitafuta huioni.
    asante.
    mdau.
    kigoma.

    ReplyDelete
  6. Duh pole sana mzee, hta ingelikua mm hapo ningekupa hyo hyo 3 japo nakuonea huruma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...