MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, utakaofanyika Jumanne ya Agosti 5, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa 10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.

Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.

“Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni waalikwa kuitambulisha taasisi.

“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation, ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.


Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tujikwamue kiuchumi na kuendeleza sehemu zote za Tanzania. Hii inchi itaendelezwa pia na mchango yetu na sisi wenyewe tukiwa na uchungu wa kuona kwetu kunaboreshwa zaidi kuliko tulivyopakuta..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...