Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Dkt. Charles Msonde kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani
Tanzania (NECTA).
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam jioni ya jana, Alhamisi, Agosti 14, 2014, na
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi huo ulianza juzi,
Jumatano, Agosti 13, 2014.
Kabla
ya uteuzi wake, Dkt. Msonde alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo hilo
la mitihani.
Dkt.
Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Joyce Ndalichako, ambaye
amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo
yake ya kujinoa (Sabbatical Leave).
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15
Agosti, 2014
Huyu Ndalichako alilaumika kwelikweli kipindiflani kumbe alikua akijinoa???
ReplyDelete