FAINALI za mashindano ya mchezo wa Pool ngazi ya Mikoa zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini(TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager zijulikanazo kwa “ Safari National Pool Competition 2014” zinatarajiwa kuendelea tena wikii hii baada ya kusimama kupisha mfungo wa Ramadhani.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga alisema mikoa inayotarajiwa kuendelea wiki hii ni pamoja na Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,Tanga na Manyala ambayo itakamilisha fainali zake mwishoni mwa wiki hii na kupata vilabu vitakavyowakilisha mikoa hiyo katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Mikoa ambayo imeshamaliza fainali za mikoa ni Lindi,Mwanza,Shinyanga na Pwani.Lindi klabu bingwa atakayewakilisha mkoa huo katika fainali za kitaifa ni Blue Leaf Pool Klabu na upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume ni Hassan Salumu na upande wa kinadada ni Mwajuma Othman, Mwanza ni Klabu ya Billiard Pool Klabu na upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume ni Lamerk Omary(Ndala Ndefu) na upande wa Wanawake ni Rukia Issa, Mkoa wa Shinyanga mabingwa ni New Stand Pool Klabu, upande wa wachezaji mmoja moja Wanaume ni Paul Filaki na upande wa Wanawake ni Sada Tullah, Mkoa wa Pwani mabingwa ni Yakwetu Pool Klabu, upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume ni Anold Djoef na upande wa Wanawake ni Fatma Kihongo.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro. Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager alizitaja zawadi za kitaifa kuwa zimeboreshwa zaidi ambapo bingwa mwaka huu atajinyakulia kitita cha pesa taslimu Shilingi 5,000 000/=.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mwendelezo wa fainali za mashindano ya Safari Pool mara baada ya mapumziko ya mfungo wa Ramadhani kumalizika.Kulia ni Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga(kulia) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mwendelezo wa fainali za mashindano ya Safari Pool mara baada ya mapumziko ya mfungo wa Ramadhani kumalizika.Kushoto ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...