Gwiji la muziki wa kizazi kipya, Alikiba, akitoa burudani kwa Wanatanga kwa wimbo wake mpya-Mwana Dar es salaam- usiku wa Fiesta Tanga, katika viwanja vya Mkwakwani jinjini Tanga.
Akiwa jukwaani, Alikiba alilazimika kuuruduia wimbo huo kwa zaidi ya maramoja kwani pindi alipoonyesha dalili ya kumaliza kuimba, mashabiki zake walipiga kelele kuomba arudie kwa mara nyingine.
Alikiba ameahidi makubwa zaidi jumamosi hii, Fiesta Moshi.
Nafurahia sana matumizi ya lugha katika nyimbo za Ali Kiba. Nimependa matumizi ya methali na misemo ya kiswahili katika nyimbo za Dushelele na hii Mwana. Aendelee kukikuza kiswahili ili watoto wetu wapate urithi wa lugha yetu. Hongera sana Ali Kiba
ReplyDelete