Naomba unipe nafasi nitoe maoni yangu kuhusu Uraia pacha nikijbu maoni yaliyoandikwa kwenye gazeti la mwananchi na bwana Humphrey Polepole. 
Maoni yake yamenishangaza sana na mtu huyu anaonekana ana hujuzi kidogo katika mambo ya uandishi na ameamua kutumua ujuzi wake kudanganya watu kuhusu swala hili la urahia pacha kwa watanzania.
Napenda iheleweke kwamba urahia pacha sio kitu kigeni Tanzania. 
Kimsingi na kimazingira Tanzania inaruhusu urahia pacha. 

1.kwa watanzania wote walio na wazazi wenye urahia tofahuti mpaka watakapofikisha miaka ishrini na moja. 
2.Kwa wanzanzibar wanye urahia wa zanzibar na urahia wa Tanzania.


Tatizo lililopo sasa ni watanzania wanataka wanufaike na urahia wa nchi nyingine pia na sio watu wengine wanufaike na urahia wa Tanzania. Hofu inayowekwa na wasiopenda maendeleo ya watanzania ni kudanganya kuwa wakongo, wamarekan, wasomali  na wengineo ndio watanufaika na urahia pacha. 
Kitu ambacho sio kweli mkongo atakapotaka kuwa rahia wa tanzania lazima aombe kupitia uhamihaji ya tanzania urahi huo. Na kira nchi inasheria zake kuhusu uraia  wa kuomba, nchi kama tanzania inabidi huwe umekaa ndani ya nchi kwa miaka isiyopungua kumi.na bado uchunguzi utafanywa kuhusu tabia zako na huko ulikokuwa kabla ya kupewa urahia wa Tanzania. 
Kwani hata ukikamilisha taratibu zote hizo bado idara ya uhamiaji inaweza kukukatila kuwa rahia wa Tanzania . Sasa ofu ya kusema wageni wengi watanufaika na  urahia wa tanzania. Inatoka wapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kabla ya ku-post makala yako jaribu ku-edit kazi yako kuna makosa mengi kama baada ya kuandika uraia unaandika urahia

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa anaanza kumcritisize mwenzake wakati yeye hajui kuandika kiswahili fasaha... matumizi ya 'R', 'L' .. 'H', 'I'.... ni tatizo MURAA

    ReplyDelete
  3. Unaongelea uraia au urahia? urahia ni kitu gani?

    ReplyDelete
  4. jamani sie tulio ndani ya nchi hilo suala la uraia pacha au na zaidi waala hautushughulishi...

    wabongo tuna matatizo mengi ya kijamii yanayohitaji utatuzi wa kudumu ila hili la uraia pacha si dhani kama lina kipaumbele

    Tango Mike - Arusha

    ReplyDelete
  5. Watanzania mbona tunazidi kubabaishana kuhusu suali hili? Inanishangaza kuona kuwa mheshimiwa rais akitukebehi tunaoishi nje ya nchi na kusema tunapoteza muda wetu kwenye blogs, lakini wakati huo huo anapokuja huku na kutuo hutba zake anasema vyengine na kuwa anakubaliana na uraia pacha. Pia vijana wadogo waliozaliwa nje ya nchi na wazazi wa kitanzania wanapewa passport za kitanzania, infact ukishuka tu uwanja wa ndege unajulishwa kuwa wanao wanaweza kupata pasi za nyumbani.
    kadhalika wazanzibari wana vitambulisho viwili vinavyoonyesha kuwa wao ni 1. raia wa zanzibar na cha 2 wao ni raia wa Tanzania.

    Wakati huo huo mbali ya kutukejeli Mheshimiwa rais ameweka kitengo cha diaspora katika serikali yake.

    Suali ni hili kwa nini tunazungushana namna hii? mheshimiwa rais ameshasema kwa kejeli kabisa kuwa hakuna uraia pacha sasa kwa nini haondoshi hichi kitengo cha diaspora?

    ReplyDelete
  6. Huyu bwana Humphrey Poleple kwa hiyo makala yake imenifanya nimuone kwamba ni mtu idealistic tu na si mchambuzi wa mambo vizuri. Hivi huyu ni msomi? Nimekuwa nafuatilia sana hoja zake za masuala ya katiba mpya na kwa upande mmoja nilikuwa nikijiuliza kwamba ni mtu idealist au anayeongozwa na uchambuzi wa mambo kitaalamu . Makala yake ya uraia pacha imenithibitishia kwamba huyu jamaa ni idelist tu. Ni wale wanaokaa macho usiku, kufikiria na ku-speculate scenarios au kutengeneza hoja kutokana na mazungumzo ya vijiweni, halafu wanaandika makala!
    (i) Ukisoma makala yake, amezungumzia masuala ya uraia pasha na kufananisha na ushabiki wa simba na yanga – kwamba huwezi kuwa shabiki wa timu mbili! Jamani kweli hii ni analogy inayoweza kutumika kwa hoja nzito kama hii! Mimi ni mnazi wa mpira kuliko mashabiki wengi wa simba na yanga lakini si mshabiki wa hizo timu mbili….
    (ii) Hoja zake za kupinga uraia pacha hazina mfano wowote wa nchi iliyopata hasara kwa kuwa na raia pacha. Namshauri yeye na wengine wanaopinga uraia pacha kwa sababu za kisalama kwa misingi ya uzalendo au hoja nyingine zozote, watoe mifano ya nchi zilizopata hasara kwa kuruhusu uraia pacha. Kama hakuna mifano ni kwa nini mnapinga uraia pacha kwa hoja rahisi na za kufikirika kama vile kusema mtu hawezi kuwa shabiki wa samba na yanga? Ukiniambia mimi nikupe faida, nitakupa nyingi tu hasa za kiuchumi ambazo zimeshajadiliwa na wengi na hata kuwekwa vitabuni. Kwa mfano soma Pickus, NMJ (Ed), “Immigration and Citizenship in the Twenty-first Century”. Wewe Humphrey Polepole na wenzako wenye mawazo kama yako kuna vyanzo vyovyote vya kitaaluma/kisayansi mnavyotumia kutete hoja zenu au ni misimamo yenu tu ya kufikirika na speculative? Unatakiwa useme kama:
    “…..tafiti mbali mbali zilizofanywa na IOM au taasisi/chuo X, zinaonesha kwamba kuna uhusiano kati ya usalama wa taifa au kushuka kwa uchumi na uraia pacha. Mifano iliyotolewa kwenye tafiti hizo ni nchi za…..”
    Usipokuwa na hoja za kisayansi halafu ukaandika makala kwenye gazeti linalotambulika, basi wewe ni cheap analyst tu mwenye malengo yako binafsi - sana sana unataka cheap popularity! Kama si cheap popularity sababu nyingine inayoweza kuwafanya mjenge hoja za kufikirika ili tu mpinge uraia pacha ni wivu kwa diaspora ambao vile vile watafaidika wao binafsi kwa uraia pacha wakati wakichangia maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Nashukuru Bwana Michuzi kwa kunipa nafasi kwenye blogg yako.
    Watu wamesoma nilichoandika kuhusu uraia pacha, na wamesikia majibu ya hoja zangu kwa mr Polepole. Najuha wote hatuwezi kukubaliana kwa hili lkn tuwe wakweli tunapolijadili na tusidangane watu wakati tunajuha tunadanganya.Kwa kumalizia ni tu naona wengi wanaokataa hawana sababu za msingi za kukataa isipokuwa wana wivu binafsi na maoni yao yanashambulia makosa binafsi sio hoja. kwa hiyo hawa ndio wana maslahi binafsi. wajibu hoja kwa hoja kama wana uwezo huo. ahasante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...