
Kuna tofauti za msingi kati ya bima inayofuata maadili ya ki
-Islam na ile isiyofuata maadili ya ki-Islam. Ktk kulifafanua hilo wataalam wa
takaful wanaeleza kwamba takaful sio mkataba wa biashara ambapo mmoja anauza na
mwengine ananunua, ispokua ni utaratibu unaopangwa na kikundi cha watu wenye
malengo yanayofanana na wakaahidi kuwa
watashirikiana endapo mmoja wao atapatwa na tatizo. Watu hao wanachanga
pesa zao (pool) kwa ajili ya malengo hayo ambapo pesa hizo zinaweza
zikazalishwa kwa faida ktk biashara ambazo ni halali kwa mtazamo wa maadili ya ki-
Islam. Kama biashara hiyo itapata faida wanagawana faida hiyo, na kama itapata
hasara basi pia wanagawana hasara hiyo. Ufafanuzi zaidi ktk tofauti zilizopo
kati ya bima mbili hizi bado unahitajika.
Tunapenda
kuwafahamisha wafuatiliaji wetu kwamba ijue bank ya kiislam imebadilika kutoka
kwenye blog na imekua website. Kufuatia mabadiliko hayo ijue bank ya kiislam
kama blog itabaki kama ilivyo lakin hakutakua na taarifa zozote mpya badala
yake wafuatiliaji wetu wanaombwa kutembelea www.ijuebenkyakiislam.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...