Naomba kutambulisha kwenu tovuti mpya ya www.kariakootz.com inayofahamika kama Kariakoo Digital ambayo imejikita katika kukusanya orodha ya maduka ya wafanyabiashara wa Kariakoo pamoja na bidhaa wanazouza, mawasiliano yao na mitaa wanayopatikana na kuyaweka sehemu moja ili kukupa urahisi wa kutafuta bidhaa unayohitaji.

Sasa unawaweza kuokoa muda na pesa zako kwa kutumia tovuti hii mpya ya www.kariakootz.com kupata orodha ya maduka mengi yanayouza bidhaa kariakoo kisha unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mwenye duka/biashara hiyo kujua/kulinganisha bei na hata kuagizia bidhaa unayohitaji ukiwa nyumbani au mikoani.

Kariakoo Digital inalenga kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kariakoo na wateja wao ndani na nje ya nchi.

Karibuni sana!


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Haya ndiyo mapinduzi ya Teknohama yanayohitajika...kama unaweza kuagiza gari kutoka Japan ukiwa Kigoma au Mtwara au pengine ukiwa Ukerewe kwanini ushindwe kuagiza bidhaa kutoka Kariakoo ukiwa maeneo hayo???kikwetukwetu zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...