Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona vitu vya ajabu vikitumwa tokea akaunti ya mtu unayemuamini sana na haukutegemea kama mtu kama yeye angeweza kutuma (post) vitu kama hivyo, na ikakufanya hata utake kujitoa (Unlike / Unfriend) toka kwenye urafiki au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.
Siku hizi, uvamizi wa akaunti kwenye Facebook umekuwa mkubwa, na asilimia kubwa ya uvamizi huu hutokana na ama wahusika kutofahamu athari wa wanachokichagua ama kutokujua jinsi ya kujilinda. Kama ilivyo ada, Dudumizi itakuelezea namna ya kujilinda na uvamizi huo kwenye Facebook.
Aina za uvamizi:
Kwenye facebook, kuna aina nyingi za uvamizi, lakini zilizo kubwa ni nne.
1) Mtu anayekujua kutumia akaunti yako (ana username na password yako)
2) Mtu asiyekujua kuotea (dictionary attack) namba za siri za akaunti yako (hii ni mra chache sana).
3) Kujiunga kwenye vipachiko (Apps) vinazonyonya taarifa zako ikiwemo password (Wengi ni wahanga hapa)
4. Kutumia computer ya mtu mwingine / asiye muaminifu
Kila aina ya uvamizi ina njia yake ya kujikinga, leo tutaangalia njia moja baada ya nyingine ambazo zitakuwezesha kujikinga na uvamizi huu.


this is great Empire ICT Solutions Co. Ltd
ReplyDeletenapenda sana michuzi blog Sofnet Solutions Ltd
ReplyDelete