Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia na kufungua rasmi Mkutano wa Diaspora.
Sehemu ya wageni waalikwa akiwemo Balozi Mwanaidi Maajar ambaye anasifika kwa kusimamia mambo ya Diaspora
Mkurugenzi wa Diaspora katika Ofisi ya Rais Zanzibar Bw. Khamis Mohamed (kushoto) pamoja na wadau kutoka ughaibuni wakifuatilia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Diaspora katika ukumbi wa hoteli ya Serena leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Mkutano wenu uwe kwetu sote najua miongoni mwenu kuna madaktari nawaombeni rudini nyumbani nchi yetu ina upungufu mkubwa wa madaktari bora kuishi kwenu mkiwa na amani kuliko kuwa wapweke ughaibuni
ReplyDeleteBongo haina kiwango cha mishahara itakayofikia malipo ya madaktari wafanyao kazi ughaibuni. Afrika bado hatujarekebisha rare professions na kiwango cha malipo yake ziwe kama sheria za kudumu za utumishi. Tuache kulaumu bali tutafute mazingira na mabadiliko ya kufikia muafaka kuona ni jinsi gani madaktari wa kiTz walio ughaibuni watasaidia nyumbani hali wakiwa ughaibuni si lazima kuwepo hapa nyumbani. Ni jukumu la wizara ya Afya kufanya jitahada za kuanzisha mchakato wa kuwajumuisha madaktari wa nyumbani na nje,kuwe na forum zao,wapate hali halisi na nini kifanyike kuboresha huduma za afya bila kugeuza kila kitu kiwe na mlengo wa siasa. Taaluma hii ni huduma ya jamii tuu. Tuwe watu wa kutenda kuliko kuandika na kulaumu kwenye mitandao. Nina hakika uliyetoa comment no.1,utakubaliana nami.
ReplyDeletemkuu Jk umeongea kweli na uwazi.Lazima turudi nyumbani tujenge nchi kwa pamoja.
ReplyDeleteuzalendo ni muhimu zaidi pamoja Tanzania haitaweza kutoa kiwango cha mishahara tunazopata huku;lakni uzalendo kwanza,nyumbani ni nnyumbani.
mimi narudi nyumbani.
Mdao wa pili umesema vizuri. Ila kumbuka nchi yetu ni maskini hayo malipo kama huku majuu ni ndoto. Ila kama mtu atajitoa kwa ajili ya nchi yake hiyo ni hiyari yake. Ila kulipwa kwa kiwango bongo ni ndoto
ReplyDeleteTangu enzi za TANU mpaka leo nasikia tu Tanzania ni nchi maskini hatuwezi kulipa mishahara ya juu , lakini watumishi kibao wa serikalai wjao huku Ulaya utaona jinsi wanavyotumia pesa ya serikali kwa matumizi ya kifahari kwa ubinafsi wao sio jumuhia . Je iweje leo Dr hapa anayepata euro 5000 Net arudi home aripwe milioni moja T schillingi(500 euro!!!) be realistic!! huyo hatafanya kazi yake kwa uaminifu ila kwa hujuma ya jamii!! fanyeni kama Ghana wakati Obasanjo alipochukuwa madaraka. Aliwawaomba wa Ghana wote waliopo popote Ulimwenguni ili mradi wamesomea kazi yoyote ulaya na vyeti na uzoeffu warudi na watapewa mkataba wa kazi mojamkwa moja baada ya kufika Ghana. N kweli waghana walirudi na wakapewa kazi na mishahara ya kuridhisha na wakaiendeleza nchi yao mpaka leo inasifika kama nchi ya kwanza africa kujikwamua umaskini kiwango cha juu bila kutegemea tu misaada ya kutoka Ulaya pekee yake au donors.!! shame us1 be creative , innovative and self constructive!! CREAT NEW COMPETATIVE IDEA AND TECHNOLOGY ACCORDING TO TIME AND gENERATION: Tuache elimu za kukariri Abort na mawazo ambayo hayaendani na muda na kiwango cha maisha na jamii.
ReplyDeleteMdau Benny S K
Germany
Very good speech. Thank you JK.
ReplyDeleteObasanjo wa Nigeiria na Ghana wapi na wapi, mdau umekaa ujerumani mpaka unachanganya marais wastaafu. Kama unalipwa vizuri huko ughaibuni kama wengine wetu basi nyumbani ni nyumbani paboreshe kwa kushiriki maendeleo ya nchi kuanzia katika kuinua familia uliyoacha nyumbani na vitega uchumi vyako vya binafsi. Usizubae au kuchezea fursa.
ReplyDeleteAcheni kutaniana, nchi yetu haijawa tayari kutumia utaalamu, sana sana wanaotakiwa kuombwa kurudi ni watu wenye asili ya ujasiliamali! Kuja kuajiriwa ni ndoto, kwani bado wako wataalamu nchini ambao tumeshindwa kuwatumia, sana sana wanakuwa frustrated! Wengi tu.
ReplyDeleteAngalia hata utaalamu wa watu kama akina Dr. Sarungi, hatukuweza kumtumia akaishia kwenye siasa, na baadae akadodondoshwa na kijana mdogo tu mwenye ujuzi wa hizo siasa. Prof. Shaba sijui yuko wapi. Tulimwacha huku tukimkejeli wakati anapata bia yake asubuhi pale along ocean road, lakini wanaojua utaalamu wake wakamchukua.
Hivyo tusitake kuwarudisha watu huku na kuja kuwaweka benchi, kumbe wangetumika vizuri kwenye dunia zinazojua umuhimu wa utaalamu.
Mnafikiri kwa nini Maprofesa wengi wamekimbilia kwenye siasa? Hakuna nafasi ya kuutumia utaalamu wao! Tuache maigizo tuwe makini na tuelewe tunataka nini na tunaelekea wapi!!
Kwa nini tusiwe wakweli? Shirika moja kubwa lilikuwa na kiongozi (RIP) aliyetaka kuwarudisha wa-TZ wataalamu kutoka nje, hiyo miiba aliyowekewa njiani kutekeleza hilo swala Muumba ndiye anayejua!
Tusipoanza kujadili mustakabahi wa taifa kwa ukweli hakika tutaangamia!
asante sana MR PRESIDENT umeongea hotuba nzuri sana...mimi naishi tanzania na sijawahi kusafiri hata kenya apo nina umri wa miaka 33 ..ni kweli ulichowaambia watanzania wanaoishi nje wawekeze wasijisahau..na kuhusu raia pacha ni kweli halitukereti sisi ilo jambo linawakera wao sasa waongeze bidii kulisema mpaka wafanikiwe mimi halinisaidii...asante sana rais WANGU ...mungu akupe afya akuepushe na wabaya amin.
ReplyDeleteyaani KATIBA ingeruhusu JK agombee tena urais mimi ningempa tena kura yangu....
ReplyDeletesiku zote watu hawaoni uzuri wako mpaka uwe haupo ...tutakukumbuka sana rais wetu JK kwa yote mazuri ulotufanyia...
demokrasia kwako ni nzuri sana tuna uhuru wa kuongea mpaka wengine sasa wanavuka mipaka na kudhihaki waasisi wetu...nakushukuru sana Mheshimiwa JK umeonyesha uzalendo wa kweli... sasa kilichobaki hao madisporaz sijui spoza wajali nyumbani wasiishie kulalamika ikiwa wao hawapo...NYUMBANI NI NYUMBANI
So turudi ili tuje kuoga vumbi ili ninyi wala vumbi mfurahi,ill keep my american citizenship no need of tz citizenship,
ReplyDeleteWe live abroad because of better living conditions,we only live once in this world and for me its easy to be happy here abroad than if i were in Tanzania, too much problems in africa ,amaong them corruption, diseases, bureaucracy etc etc
ReplyDeleteHuyu mdau wa mwisho anayesema bongo ni matatizo akili zake hazina akinli. Yaan unafurahia maisha mazuri kwa wenzako unasahau hao wanaopata shida ni ndugu zako na wanahitaji msaada wako wa hali na mali hata kimawazo tu kujikwamua na matatizo yanayowakabidhi? Shame on you.
ReplyDelete