Akiongea na waandushi wa habari Ofisini kwake, NAIBU KATIBU MKUU TAIFA NA KATIBU WA BODI YA CHAMA (NRA), mhe HASSAN KISABYA ALMAS, amewaonya viongozi wenzake wa kisiasa kuacha malumbano na badala yake wajikite kuhakikisha Taifa linapata katiba,
Mhe Kisabya alisema, "mpaka sasa wajumbe wa bunge wanasiasa wamekuwa wakijadili nafasi za kisiasa za utawala na kusahau kuwa kuna mambo mazuri muhimu yanayohusu wananchi"Akitoa mfano kuwa suala la idadi ya SERIKALI ni jambo la kuamua lakini masuala kama Tume huru ya UCHAGUZI, suala la mawaziri kutokuwa wabunge, haki za binadamu,mahakama huru,kupungua kwa madaraka ya Rais , matokeo Rais kupingwa mahakamani na haki ya umiliki wa ardhi, haki za wakulima na mengine mengi ni baadhi ya mambo muhimu kwa ukuaji wa demokrasia na maendeleo ya wananchi, mhe Kisabya alishauri kuwa suala la Katiba ni suala nyeti hivyo viongozi wenzake wa vyama walichikulie kwa umakini na kulipa uzito wa kipekee.
Ndugu Kisabya aliongeza kuwa , ikiwa Katiba hii itakwama basi watanzania wajipange kuwaadhibu baadhi ya wanasiasa kwa kuwanyima kura katika chaguzi zijazo,"ikiwa sisi wanasiasa Ndio tuliokuwa kila siku tunadai katiba iweje Leo Sie Ndio tuwe mstari wa mbele kugomea, ama sivyo hatukuwa wamoja katika kudai katiba Bali wengine walikuwa na ajenda zao"
Mhe kisabya alisema, kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba inaelekeza kuwa ,iwapo katiba hii mpya itakwama basi tutarejea kuongozwa na katiba ya mwaka 1977;katiba ambayo tumekuwa tikiikataa kuwa inatunyiwa wigo wa kidemokrasia.
Mbali na taarifa pia mhe kisabya aliwaeleza wanahabari kuacha kuiandikia mabaya ya Tanzania na kuvisifia vyama vya siasa kwa kuwa Hakuna chama nje ya taifa, na vyama vinaweza kuondoka ila taifa litabaki ,hivyo hakuna chama kinaweza kuwa na umaarufu kuliko taifa, na kusisitiza kuwa NRA inaamini kuwa sera yake ya Taifa Kwanza vyama baadae ni msingi wa AMANI ya taifa hili, kwani wao wapo tayari kukosa nafasi za utawala ilimradi Usalama,umoja wa taifa na mshikamano wa watanzania na utulivu wa Taifa ubakie imara.
Kuhusu, CHAGUZI ZIJAZO, NRA wamejipanga kusimama katika chaguzi za SERIKALI za mitaa na chaguzi Kuu ya mwaka2015 katika nafasi zote za udiwani, ubunge na Urais kwa kusimamisha watu Makini wanaokubalika na wananchi.alisema, NRA inategemea kuvuma watu maarufu kuelekea 2015 watakaogombea nafasi mbali mbali.
Pia mhe kisabya, aliwaeleza wanahabari kuwa NRA , itaandaa kumbukumbu ya kuwaenzi waasisi wake, Hayati Prof. Kighoma Ali Malima na Hayati Aboubakar Ulotu ,maandalizi yake yanaendelea.
Mhe kisabya, alimalizia kwa kuwataka wabunge wengine walio nje ya bunge kurejea bungeni kumalizia kazi waliyoianza vizuri ,na kuwasisitiza kuwa wanayo nafasi ya kusimamia fikra zao wakiwa bungeni na watanzania watawasikia ili kupata mwisho mzuri, alisema nchi haitapenda kuona damu za watanzania zikimwagika kwa ajili ya katiba hii Bali katiba hii iwe ni chanzo cha maendeleo amani na utulivu wa taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...