Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akiongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Taifa ya Maafa(TANDREC) ambayo, inaundwa na Washiriki wakuu katika kukabili Maafa, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Dharura na Maafa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Elias Kwesi, akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) jinsi walivyojidhatiti kuzuia na kukabili ugonjwa wa Ebola hapa nchini ambapo alibainisha kuwa hakuna maabukizi ya ugonjwa huo hapa nchini hadi sasa, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kumaliza kikao hicho leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...