Na  Magreth Kinabo- MAELEZO

Baraza la Vyama vya Siasa nchini  limeamua mazungumzo  ya maridhiano  kati ya pande zinazokizana kuhusu kuendelea kwa  Bunge Maalum la  Katiba  kutokana na mvutano  wa kutaka serikali mbili au tatu  yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa.

Aidha baraza hilo,limeamua kufanyike kongamano Agosti 9 na 10 mwaka huu mjini Dodoma kwa  ajili  ya kuangalia maslahi mapana  ya taifa.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter  Kuga  Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.

Alisema katika mkutano huo,  baraza hilo limepokea ripoti ya mkutano wa  Msajili wa Vyama Vya  Siasa nchini na baadhi viongozi wa vyama vya siasa, pia limepokea ripoti ya chama kimoja kimoja, ambavyo ni Chama cha Demokrasia  na Maendeleo ( CHADEMA), Chama  cha Wananchi (CUF)  Chama cha NCCR – MAGEUZI na Chama cha Mapinduzi (CCM).

 Aidha  Mziray  amesema  kwamba  katika mkutano huo, kuna mambo ambayo wamekubaliana na mengine hawakuafikiana.

 “Baraza limeamua mazungumzo ya mariadhiano yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa ,ambazo zitakuwa na wajumbe wachache. Baraza linawashauri wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba warudi Bungeni  kwa kuwa ndio mahali pekee pa kutoa hoja na wala si sehemu nyingine,” alisema Mziray.

 Aliongeza kuwa anavipongeza vyama hivyo kwa kuonesha nia ya kuendelea kwa mazungumzo hayo na  wameonesha imani na baraza hilo, ambapo wametaka majadiliano  kupitia kamati yafanyike.

 Mwenyekiti huyo akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya  Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika, viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini zote.

“Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano  katika suala hili. Tunategemea busara za viongozi hawa zitatubadilkisha  na kutuweka pamoja  kwa maslahi ya taifa na kuachana na mambo ya kivyama,” alisisitiza.

Aliyataja mambo ambayo, wamekubaliana kuwa yasiwepo wakati wa kuendelea kwa Bunge hilo ni kutumia lugha za matusi na kejeli.

Katika  mazungumzo hayo, “Baraza limeona   si rahisi kufikia muafaka kwani kila upande  ulionesha kuwa Bunge hilo halina mamlaka ya kubadilisha Rasimu ya  Katiba Mpya, na mwingine unadai Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha na kuboresha rasimu hiyo kwa vile  suala hilo lipo kisheria kulingana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kifungu cha 25 na kanuni zinaruhusu,” alisema Mziray.

Kwa upande mwingine Mziray  alisema kuwa jambo lingine lilionesha ugumu ni mvutano uliopo wa kuhusu wa kuwepo kwa Serikali mbili au tatu kwa sababu ni  suala la kisera za vyama na sera haibadilishwi mpaka mkutano mkuu wa chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. The mdudu,vikao kaeni hata vikifika 10 lakini serikali 3 sio ombi bali ni lazima coz nimaoni ya wananchi walioyatoa kwenye tume ya Walioba ili kuondokana na UMANGI MEZA WA VIONGOZI MCHWALA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tusifuate mawazo ya wanasiasa watatutumbukiza kwenye matatizo. Tatizo hapa sio serikali mbili au tatu tunataka Katiba bora inayotekelezeka.

      Delete
  2. Swali la Msingi hapa ni hili : Je,inawezekana kwa Taifa Moja kuwa na Serikali Tatu ? Jibu , ni Ndiyo inawezekana . Je,serikali hizo tatu zitakuwa na Muundo upi , zitafanyaje kazi kwa pamoja ili kuhakikisha Taifa Moja halisambaratiki ? Kwa vipi serikali hizo tatu zitaweza kudumisha Umoja wa Kitaifa ? Swali lingine la kujiuliza ni hili : Je,inawezekana kwa Serikali Moja kuwa na Mataifa Matatu tofauti ? Jibu ni kwamba , hilo haliwezekani. Tumekuwa na muundo wa serikali mbili kwa miaka yote iliyopita.Tumeshaona mapungufu yake,hatuwezi tena kuendelea na mfumo uleule wa serikali mbili katika mazingira mapya ya vyama vingi vya siasa .Tutahitaji Mabadiliko.Na mabadiliko hayo , ni Katiba Mpya iliyopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba.Mapendekezo hayo yatafanyaje kazi,ndiyo kazi inayolikabili Bunge la Katiba.Na siyo kuja na Rasimu Mpya tofauti na iliyo wasilishwa na Tume ya Katiba.Vinginevyo , zoezi zima itabidi lianze upya kabisa , na tofauti na ilivyo sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...