Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania limesema kwamba kongamano la kujadili chakato wa kutunga Katiba mpya na changamoto zake lililopangwa kufanyika Agosti 9 na 10 mwaka huu limesogezwa mbele, hivyo litatangaza tarehe ya kufanyika.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Mziray katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mjini Dodoma leo.
“Kutokana na uzito wa kongamano hilo na kazi kubwa ya maandaliziyake, inayotokana na uwingi na uzito wa wageni waalikwa, kongamano hilo halitafanyika siku ya tarehe 9 na 10 Agosti, mwaka 2014 kama lilivyopangwa awali. Hivyo basi tarehe ya kufayika kongamano hilo imepelekwa mbele na baraza litatangaza,” alisema Mziray.
Aliongeza kuwa kongamano hilo litakuwa tukio kubwa na muhimu kwa nchini yetu, kwani litajadili kwa kina mchakato wa kutunga Katiba mpya unaoendelea na changamoto zinazoendelea kukabiliana nazo.
“ Wadau wote wanaohusika na mchakato huu wataalikwa na watoa maoni yao,” alisisitiza.
Aidha Mziray alisema kongamano hili litaibuka na maazimio ambayo, baraza hilo, linaamini yatakuwa na uzito na ushawishi katika mchakato huo kwa kuwa yatazingatia maslahi mapana ya taifa, hali halisi ya siasa, uchumi, utamaduni, jamii na haja ya kudumisha Muungano wetu na hatima ya nchi kwa miaka mingi inayokuja.
Awali akizungumza na waandishiwa habari hivi karibuni jijini Dares Salaam kufuatia kufanyika Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Kuga Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.
Mwenyekiti huyo akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika, viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini zote.
“Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano katika suala hili. Tunategemea busara za viongozi hawa zitatubadilkisha na kutuweka pamoja kwa maslahi ya taifa na kuachana na mambo ya kivyama,” alisisitiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...