LIGI ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kaunza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya  Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.

Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni moja ya mkakati wao wa kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.

Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri Queens,  Simba Queens,  BYC Queens, JKT Queens,  Lulu Queens,  Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni Queens.

“Kwa kweli ligi ya wanawake nayo ni muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi yao na sisi tunaona hili ni jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa (Twiga Stars).

Mharizo aliyaomba makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili iweze kuleta ushindani kwa timu shiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...