Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Maaskofu
wa Kanisa la Moravian nchini baada ya kuwasikiliza malalamiko yao kuhusiana na migogoro
ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea kwa muda mrefu katika Kanisa hilo. Maaskofu hao
ambao walikuwa wanaongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Alinikisa Cheyo walimuomba
Waziri Chikawe aingilie kati kwa kudhibiti vurugu hizo ambazo zinazisambaratisha kanisa lao.
Hata hivyo, Waziri Chikawe aliahidi kulifanyia kazi suala hilo na atalitolea maamuzi baada ya
kufanya uchunguzi wa kina kwa kukutana na pande zote mbili zinazogombana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini
Askofu wa Kanisa la Moravian nchini, Conrad Nguvumali (watatu kulia) wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo. Maaskofu
watano wa Kanisa hilo ambalo limekumbwa na mgogoro kwa muda mrefu sasa, wakiongozwa
na Askofu Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Alinikisa Cheyo (wapili kushoto) walionana na
Waziri huyo ili kuomba msaada wake katika kudhibiti vurugu zinazoendelea katika Kanisa hilo.
Hata hivyo, Waziri Chikawe aliahidi kulifanyia kazi na hatimaye kulitolea maamuzi suala hilo
baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kukutana na pande zote mbili zinazogombana. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa kweli Bwana yesu awasamehe badala ya kumuambia roho mtakatifu aingilie kati kuleta amani ndani ya kanisa mnamuambia binadamu aingilie kati. Huduma hiyo mmeitwa na Mungu kweli hata kukosa ufahamu huo wa kutambua nani asululishe?
ReplyDeleteWafanyabiashara hao hawana roho mtakatifu, Watu wa Mungu hawawezi kugombana mbele ya nyumba ya bwana.
ReplyDeletehata mimi nilipoona ili nikawaza siasa za nini kanisani?
ReplyDeletekwanini wenyewe viongozi na waumini mnashindwa kujadiliana na kupata ufumbuzi?