Mameya na Wakurugenzi wa majiji sita ya Tanzania walioko katika ziara ya mafunzo nchini Finland wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa jiji la Helsinki,Hannu Pentila muda mfupi baada ya viongozi hao kutembelea mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Kalasatama katika jiji hilo la Helsinki.
Ujumbe wa Mameya na Wakurugenzi kutoka majiji sita ya Tanzania ukitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa katika mji wa Kalasatama jijini Helsiniki nchini Finland.
Lisa Tervo kushoto kutoka Taasisi ya Uongozi ya Tanzania akitoa maelezo kwa Naibu Meya wa jiji la Helsiniki Hannu Pentila huku Godfrey Nyamurunda (wa pili kushoto) wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania akishuhudia
Baadhi ya majengo katika mji wa kisasa wa Kalasatama, Helsinki.
wakirudi warudi na kitu angalau,sio kwenda kushangaa magorofa
ReplyDeleteMuende mujifunze halafu muje mtupangie miji yetu mikoa na wilaya. Sito kwenda tu study tour halafu mafunzo waliyopata hayabadilishi chochote.
ReplyDeleteNakubaliana nawe Anony namba 1.
ReplyDeleteTunatumani mtarudi na mengi ya kuwaletea wananci, Kuna mengi sana ya kujifunza, kwa haraka haraka, Kwanza, miji yao ilivyo safi, Pili hakuna nyaya zimekatizakatiza hovyo!, tatu, hapo mlipopigia picha si lami ni vile vitofari vidogo vidogo vyatosha kutengeneza barabara za mitaa na miji ikawa safi bila lami feki wala ujenzi wa kiwango cha lami. Kazi njema, tunategemea mabadiliko.