Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa Salaam Dk Didas Masaburi.
 Baadhi ya viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa taka na uchujaji wa maji machafu katika jiji la LAHTI, kutoka kushoto ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania, ( Tanzania Cities Network) Philoteus Mbogoro, Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi, Lissa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania, Johanna Palamoki ambae ni mtaalam wa mipangomiji katika jiji la LAHTI, Mkurugenzi wajiji la Lahti Kari Porra na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga ( picha zote na Vedasto Msungu wa ITV)
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
 Viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakiwa kando kando ya ziwa Maji ambako mkondo wa maji machafu kutoka majumbani huingia ziwani baada ya kuchujwa, viongozi hawa kutoka kushoto ni Stanslaus Mabula ambaye ni Meya wa jiji la Mwanza, Athanas Kapunga ambae ni meya wa jiji la Mbeya, Mussa Zungiza,mkurugenzi mtendaji wa jiji la Mbeya na Philoteus Mbogoro ambae ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania TACIN
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. tanzania kuna mchwa sana sasa kujenga na mbao ni kuzuri lakini mchwa je?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...