Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma waliohudhuria katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanayofanyika mkoa huo wakikabidhiwa vipeperushi na Afisa Utawala wa Baraza la Ushauri wa Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania,Catherine Monarya, wakati walipotembelea banda la TCAA.
Fundi wa mitambo ya Kuongozea ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Mkiramweni akiwaelezea wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lukundo ya mjini Dodoma Redio ya kuongozea ndege wakati ianapokuwa angani, wakati walipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya NaneNane Kanda ya Kati yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akiwaelezea baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma shughuli zinazofanywa ma mamlaka hiyo wakati walipotembelea banda lao kwenye maonesho ya Nanenane kanda ya Kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Akina mama wakazi wa mkaoa wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini Afisa wa Hali ya Hewa Juma Binda wakati alipokuwa akiwaelezea jinsi wanavyopima mvua ,wakati walipotembelea banda hilo lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayfanyika katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma Maonesho hayo yamebeba ujumbe wa ‘’Matokeo Makubwa sasa “Kilimo ni Biashara.
Afisa wa Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) Francis Mariwa akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lukundo juu ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo wakati walipotembelea katika banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.Maonesho hayo yamebeba ujumbe wa “Matokaeo Makubwa sasa”Kilimo ni Biashara.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao walifika katika maonesho ya Nanenane wakimsikiliza kwa makini Afisa Uhusiano na Masoko wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Monica Mutoni wakatialipokuwa akiwaelezea juu ya shughuli mbalimbali za hari ya hewa wakati walipotembelea katikabanda lao kwenye maonesho ya Nanenane yanaoyendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...