Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imezindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa
Watu kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa Mtwara, zoezi ambalo litadumu kwa siku
14 kuanzia Jumatatu tarehe 18/08/2014.
Akizungumza katika sherehe fupi ya
uzinduzi wa zoezi hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho;
ndugu Joseph Makani amesema kuanza kwa zoezi hilo Mtwara ni utekelezaji wa
mpango wa Usajili wa wananchi na wakazi waishio kihalali nchini wenye lengo la
kuwapatia vitambulisho vya Taifa Raia, Wageni na Wakimbizi baada ya zoezi kama
hilo kukamilika wa wananchi wa Tanzania Zanzibar, mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani
na sasa Mtwara.
Amesema ufanisi
wa zoezi hilo unategemea sana ushirikiano toka kwa viongozi katika serikali,
vyama vya siasa na viongozi wa Dini ambao walikuwepo kushuhudia tukio hili.
Naye mgeni rasmi kaimu Katibu Tawala Mkoa ndugu Jehasen Bukwali kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ameahidi kutoa ushirikiano na kusimamia kwa dhati zoezi
hilo kufanyika katika mkoa wa Mtwara, huku akiwataka viongozi katika ngazi zote
kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi la Usajili ambalo linamatokea
makubwa katika ustawi na maendeleo ya Taifa.
Amewaasa
wananchi na wanasiasa kutohusisha zoezi hilo la Siasa, kwani vitambulisho vya
taifa havihusiani na itikadi za chama chochote, na haki ya kila Mtanzania
kusajiliwa na kupata haki yake msingi kikatiba.
Ufunguzi huo
uliwakilishwa na viongozi katika ngazi za juu Mkoa, na Wilaya zikiwemo kamati
za Ulinzi na Usalama. (picha na Rose Mdami (NIDA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...