BENDI ya Masai Safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa watakayozindua siku ya  Agosti  30, mwaka huu  katika ukumbi wa Lunch Time,  Tip Top Manzese jijini Dar.
Akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki.
Alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.
aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi huo.
Bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...