![]() |
Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso . |
![]() |
Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya Lori la mafuta. |
![]() |
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo. |
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii
kanda ya Kaskazini.
Ajali mbaya imetokea barabara kuu ya
Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Sacania lenye namba za Usajili T
137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya
Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini
Moshi(MUWSA).
Mashuhuda wa ajali hiyo
waliiamia Globu ya Jamii kuwa ilitokea majira ya saa 7 katika makutano
ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo chuo cha polisi Moshi
kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.
Katika ajali hiyo mwndesha pikipiki
aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya, mfanyakazi wa Mamlaka ya
maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, alifariki dunia papo
hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...