Katibu Mtendaji Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Jukwaa la Wadau watakaoangalia mazao ya
mikunde na nafaka litakalofanyika Agosti 20 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo na Ofisa Programu wa Women & Youth Development Foundation, Luke Daniel Kifyasi.
Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Na Clezencia Tryphone
Waziri
Mkuu Pinda, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la wadau watakaoangalia
mazao ya mikunde na nafaka mara baada ya kuvunwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge amesema katika uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip Agosti 20 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi.
Alisema lengo la kufanya uzinduzi huu ni kutokana na changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanyabiashara kwa
ujumla.
Miongoni mwa changamoto hizo, ni utuzwaji wa mazao
hayo baada ya kuvunwa, hasa kwa wakulima wadogo wadogo na wale wa kati na
wafanya biashara huku changamoto nyingine ikiwa ni upotevu wa Mbegu pamoja na
matumizi ya tekinolojia ya utunzaji na takwimu.
“Tunatarajia kufanya uzinduzi wa jukwaa la wadau
wanaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara tu baada ya kuvuna, na lengo kubwa
ni kuwaamasisha pia watunzaji wa nafaka hizo, ili kuepuka upotevu, na tumefikia
hatua hii baada ya kufanya utafiti,”amesema Rukonge.
Amesema, mara baada ya kufanywa kwa takwimu wamegundua
kuwepo kwa upotevu mkubwa wa mbegu za mazao hayo na hiyo ndiyo sababu
iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...