Balozi Mdogo wa Tanzania-Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa benki ya UBL ya Dubai,Bw. Shaikh Muhammad Liaque, Makamu wa Rais wa UBL (kushoto) na Bw. Syed Abbas Bokhari walipomtembelea ofisini kwake leo.
Wakiwa katika mazungumzo,ambapo Mhe. Mjenga amewaomba kuangalia uwezekano wa kuajiri Watanzania kwenye Benki hiyo kuja kufanya kazi Dubai. Mwaka jana, UBL ilifungua ofisi zake jijini Dar es salaam. Mh. Mjenga amewaomba pia kuifanya ofisi ya Dar es salaam kuwa ofisi ya Kanda ya Afrika. Aidha, wamegusia suala la kufungua matawi zaidi Arusha, Moshi, Mwanza, Mbeya na Matawi mengine zaidi Jijini Dar es salaam. Hii yote itafanikisha kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...