Paulina Nyoni (Mama wa mtoto Fatuma Msuya) akiwa amembeba mwanaye ambaye anahitaji msaada wa matimabu .

----------------------
Paulina nyoni mkazi wa kijiji cha Hanga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa na tatizo la mwanaye  aitwaye Fatuma Msuya ili aweze kupata matibabu katika hospitali ya KCMC moshi.

Paulina ni mama mwenye watoto wa tano anayejishugulisha na kilimo , Mume wake aitwaye  Jafari Msuya amemtelekeza baada ya kujifungua mtoto mwenye tatizo hili na kukimbia kusikojulikana hivyo kumfanya mama wa mtoto huyu kutokuwa na msaada wowote ule,

Fatuma Msuya (1) amezaliwa tarehe 24/2/2013 katika Hosptali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na tatizo la kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji tumboni ambapo kwa sasa anatolea haja kubwa,awali kabla ya kupasuliwa alikuwa akitolea haja kubwa sehemu ya aja ndogo.

Upasuaji wa awali alifanyiwa katika Hospitali ya Mission Peramiho iliyopo wilaya ya songea tarehe 19 04/ 2013
Na kwa sasa mtoto huyu anakabiliwa na tatizo jingine la kutokwa na vidonda sehemu anayojisaidia  hali inayomsababishia maumivu wakati wote na anapojisaidia haja kubwa hutokwa na damu.

Gharama za matibabu zinazohitajika  ni shilingi milioni tatu, Yeyote atakayeguswa anaweza kutoa msaada kwa Mpesa no 0767 710 113 .
“Kutoa ni moyo”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani Jamani tatizo kama hili serikali iko wapi? Mtoto Mdogo kazaliwa na tatizo; tena kazaliwa katika hospital ya serikali halafu wanamwachia mama atoke nae hospital kwenda nyumbani? Kama kweli serikali inaangalia na kuwajali watu wake basi imjali na huyu mtoto; million tatu kwa serikali ni nini jamani? Mheshimiwa Mwambungu mwangalie huyo mtoto! !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...