Mtangazani Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.

Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. 

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio. 

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Du pole zake! kweli pombe sio chai. Inatakiwa maneno yake redioni na matendo yake viendane. Mtu mzima hovyooooo!

    ReplyDelete
  2. Ukimsikia Kibonde akipiga vita ulevi kwa madereva, mbona utachoka.

    ReplyDelete
  3. Hii ni tabia ya kawaida siku hizi katika barabara za Tanzania, sina uhakika kwa majirani zetu kukoje! Mtu anafanya anavotaka barabarani. Pole Bwana Kibonde kwa yaliyokukuta lakini liwe fundisho kwa watu kuheshimu taratibu tulizojiwekea, la sivyo barabara zetu zitaendelea kuwa machinjio!

    ReplyDelete
  4. Haya ndiyo matatizo ya ulevi wa kijinga. Huyu inabidi apewe mkong'oto wa nguvu ajifunje vizuri, pumbavu kabisa alafu eti anawekwa kwenye matangazo ya kuelimisha jamii...phuuuu!

    ReplyDelete
  5. Asiposhitakiwa na kufikishwa mahakamani nitaamini kweli polisi kuna rushwa.

    ReplyDelete
  6. Ulevi nouma! Hata mtu maarufu kama Kibonde analewa na kufanya maajabu... Lakini cha ajaabu ktk nchii hii wenye hela zao wata'sevu' atapewa faini ya 20,000 atarudi mtaani akitamba

    ReplyDelete
  7. Huyo jamaa kwa kweli ni bwege sana. Ukimsikia kwenye Radio na majigambo yake utafikiria kuwa yeye ni mtu msafi kwa matendo na mienendo yake kumbe bure kabisa hafai ata kuigwa . Sasa namshauri aende akamuombe radhi Mkewe na wanawe kwa kuwahaibisha.

    ReplyDelete
  8. Assalam aleyka kibonde

    ReplyDelete
  9. kaka tulizana,hizo pombe huchelewi kuchepuka harafu ikawa aibu...

    ReplyDelete
  10. Kuna mdau anasema ni act ya kufundisha watu kutii sheria bila shurti

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaaaaaa. Act indeed

      Delete
  11. Acheni kudanganya watu nyinyi juzi walipigana studio leo eti kakamatwa kwa kukaidi amri ya polisi kisa kagonga gari ya watu msitufanye watanzania sisi ni majuhaa wa kudanganywa

    ReplyDelete
  12. Haya maelezo ni kwa mujibu wa nani? Tunaomba tujue yasiwe kama yale ya Jerry Muro.

    ReplyDelete
  13. Huyu jamaa ni pumbavu he needs to be hit hard with the Law.. please prosecute him..!

    ReplyDelete
  14. Du, Kweli huyo kibonde. Polisi wetu ni wastaarabu hivyo, au kwa vile ni celebrity? Maana jeuri yote hiyo, hawajamtoa manundu!

    ReplyDelete
  15. ISIWE SHIDA. HUYU KACHEPUKA TU...!!!!

    ReplyDelete
  16. Kijana hajatulia kabisa.

    ReplyDelete
  17. Hajiheshimu huyo.

    ReplyDelete
  18. Najua wajua lakini nataka kukujuza zaidi Kibonde alikuwa location akirekodi filamu itakayojulikana kama 'The Weekend Disaster'

    ReplyDelete
  19. Kichwabuta MuchwampakaAugust 10, 2014

    Shame on him (KIBONDE) !!!, and those using this chap for their adverts should thoroughly weigh if they do like their adverts be of value in the NATION ! He has shown his TRUE character to the ever emerging society ! Poor KIBONDE !!!!!

    ReplyDelete
  20. Nayeye atashitakiwa kwa kumteka polisi au la! Maana hili tukio linafanana na habari niliyoisoma humu ya jamaa kumteka askari polisi.

    ReplyDelete
  21. Tunaomjua wala hatupati shida. Anapenda sana, pale alipo hutaka watu wote wajue yeye upo. Kapatikana, na hiyo itakua gongo tu. Beer asingefanya hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...