Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana amezindua mradi mkubwa wa maji wa Mambogo, mkoani Morogoro, katika ziara yake aliyoainza juzi mkoani humo. 
“Napenda kumshukuru Rais Obama na Serikali ya Marekani kwa ushirikiano mzuri na nchi ya Tanzania, hasa katika kuleta maendeleo na pia Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC na MCA-T) ambao wamekua wadau wazuri wa maendeleo nchini katika sekta mbalimbali na sio maji pekee”, alisema Rais Kikwete. 
“Ni kazi kwetu sisi kuutunza mradi huu mkubwa wa maendeleo na kuutumia vizuri ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa na MORUWASA haina budi kuzingatia hilo. Huku ikishirikiana na viongozi wa mkoa kuhakikisha maji yanakua si tatizo tena”, alisema Rais Kikwete. 
Aidha, Mhe. Kikwete aliwaasa viongozi kuwa makini na utunzaji wa vyanzo vya maji kwani ndio muhimu na bila vyanzo hivyo, upatikanaji wa maji utakuwa mgumu kutokana na upungufu wa rasilimali hiyo. 
Aliendelea kusisitiza viongozi kutokua waoga katika kuchukua hatua na kusimamia rasimali hizo kwa nguvu zote bila uzembe. 
Aidha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba alisema utekelezaji wa mradi huu ni hatua kubwa ya kuboresha upatikanaji na ubora wa maji kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, na kwamba  utaleta manufaa kwa wakazi wa Manispaa wanaotumia huduma za majisafi kutoka vya maji vya Bwawa la Mindu na Mambogo. 
Pia, Inj. Futakamba aliongeza Wizara yake imetenga fedha kiasi cha Sh. Mil 400 kwa ajili ya kupanua mtandao wa maji ili wananchi waweze kuunganishwa kwa wakati katika mwaka wa fedha 2014/15. 
Mradi wa Mambogo ni moja ya miradi mikubwa nchini, unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro (MORUWASA), unategemewa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka meta za ujazo 23,000 kwa siku hadi meta za ujazo 33,000 kwa siku katika kuhakikisha tatizo la maji mkoani humo linapatiwa ufumbuzi, huku wananchi wengi wakitegemewa kuunganishwa kwa haraka kwenye mtandao wa maji katika Manispaa hiyo. 
Mradi huo umedhaminiwa na Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC na MCA-T) ), ukiwa ni moja ya malengo ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo huduma za jamii, ikiwemo seakta ya maji. 
Mhe. Kikwete yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya siku nane akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa maji wa Mambogo mkoani Morogoro ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Sehemu ya jengo la mradi huo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king'ora kuzindua rasmi mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine wakielekea kukagua  mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...