Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha noti bandia zilizokamatwa

Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 


Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.
Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kuweka mtego ambapo askari walifika katika eneo hilo na kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na noti hizo bandia zilizokuwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri. Aidha watuhumiwa walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia. 
Watuhumiwa hao ni:-
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.RICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPHREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sasa si noti bandia za marekani
    sie zinatuhusu??? wapeni zigo lao waende zao marekani!!

    ReplyDelete
  2. Hii ni aibu, japo siyo hela zetu,kama wanafanya hivi je tuna uhakika gani hawaja fanya hivibkwa hela zaki Tanzania ? Lazima tujali haya maswala. Huu mtizamo wa kutojali matatizo madogo umeshazua matatizo mengi sugu.
    Ona sasa vijana wetu wameolewa na pombe, madawa ya kulevya na mengineo na mbaya. Hakuna mtu anaweza kudai kuwa hapakuwa na dalili za tatizo na pia kuwa wahusika wangeweza kustishwa ikiwa kama jamaa tungesimama pamoja na kusema : fulani unapotea! Acha hayo. Siku hizi kila mtu hana muda, na kila mtu anilia mwenyewe kuwa kijana anamatatizo. Kama jamii tusione tatizo na kunyamaza, kunyamaza ndiyo kumezaa matatizo sugu ya nchi yetu. Amkeni tuache kulala, tusipalilie matatizo, tayang'oe yanapo anza tu. Japo halionekani ni kubwa litaota tu na litaja umiza wengi. Washughulikiwe wano na wafadhili wao !

    ReplyDelete
  3. Sheria iwashughulikie ili liwe funzo kwa wengine kuwa ni makosa kutengeneza noti bandia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...