Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro,Mhe. El-Anrif Said Hassane amekabidhi rasmi eneo lililototewa na Serikali ya Comoro kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni. 

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Wizara ya Mambo ya Nje ya Comoro ambapo Mhe. Waziri El-Anrif amemkabidhi Mhe. Chabaka F. Kilumanga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro, funguo za majengo matatu yaliyopo katika eneo hilo. Tukio hilo lilishuhudiwa pia na Mhe. Ahamada El-Badaoui Mohamed Fakih, Balozi wa Comoro nchini Tanzania.

Sambamba na kukabidhiana eneo hilo, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Waziri El-Anrif walipata fursa ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka F. Kilumanga (katikati) akionyesha funguo aliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro,Mhe. El-Anrif Said Hassane (kulia) ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa eneo lililototewa na Serikali ya Comoro kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka F. Kilumanga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro,Mhe. El-Anrif Said Hassane

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ingawa mimi si mwanadiplomasia, naomba kusema yafuatayo:

    *Caption ya picha ya kwanza kinasema tumepokea eneo kwa ajili ya "ujenzi" wa ubalozi wetu

    *Habari pia kinasema Balozi wetu amepokea funguo za majengo matatu.. kwa hiyo, je, hii ina maanisha tutazibomoa na kujenga jengo kipya?

    *Kama ni eneo tu, basi wangempa hati za umiliki [title deed] kama ishara ya kukabidhi.

    *Naomba nitoe ombi kwa ubalozi wetu, watuwekee picha za hizi jengo 3 na ya eneo la ubalozi wetu. Pia, itagharimia bilioni ngapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...