Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam  na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO  kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo,bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi  wa eneo hilo.

Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.

Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda


Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...