Blog ya Swahilivilla Siku ya Jumamosi July 19 2014 ilifanikiwa kufanya Mahojiano na mtaalamu wa uchumaji wa mauwa ya asumini Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa, a.k.a (Kijakazi) ambae alielezeaa mengi kuhusu umuhimu wa Asumini pamoja na utunzani wake.

Mtaalamu wa uchumaji asumin Alwatan Kijakazi Hassan Mustafa akiwa katika harakati za uchumaji wa mauwa ya yenye harufu nzuri asumin.
Katika Mahojiano haya na mtaalamu wa utunzaji wa Miasumini Kijakazi Hassan Mustafa ambae ni mkaazi wa Mwembetanga Zanzibar atuelezea mambo mbali mbali kuhusu umuhimu wa ujumaji na utuzaji wa mauwa ya Asumin, ya kiwemo kusingwa kwenye sherehe za harusi na hata kutengezea uturi pamoja na vikuba vyenye harufu nzuri ya kunukia.
Asumini ni BUSTANI ya mapenzi yenye mauwa madogo yenye kutoa harufu nzuri, huchumwaa kwa kuwekewa kitandani ili bwana asitoke ndani wakti muwafaka wajioni.
Kwa mawazo zaidi wasiliana nasi kwa njia ya Email: swahilivilla@gmail.com
Ungana nasi taratibu kusikiliza mahojiano haya.
Masha Allha Bi Kijakazi umetufahamisha uzuri khabari nzima kukhusu 'Asumini' khususan faida na matumizi yake kwa jumla. Binafsi nimepata kufahamu kuwa, siyo tu tukiwa hai peke yake ndio tunazitumia Asumini, la khasha! kumbe hata mja anaporejea kwa MOLA wake (akishakufa), mchanganyiko wa unga wa asumini, viluwa, mirehani n.k. hutiliwa maiti katika Sanda yake ili anukie uzuri. Hongera sana Da Kija (Da Kijakazi) pamoja na muongozaji wa mahojiano haya, lugha fasaha mliyotumia na mtiririko mzuri wa maneno kama inavyostahili katika mahojiano. Nawatakia na kuwaombea kila lenye kheri katika shughuli zenu za kila siku na Mwenyeez Mungu awalinde kwa kila jambo.
ReplyDelete