Na Sultani Kipingo
Anajulikana kwa kutumbua maraha na kuishi kifahari, lakini rapa milionea Snoop Dogg ameacha gumzo huko Uingereza kwa kukaa katika hoteli ya bei ya chini ya Holiday Inn Express wakati wa onesho lake katika kitongoji cha Devon, Exeter, wikiendi ilopita
Msanii huyu wa Marekani, ambaye alilipwa pauni za Uingereza 22,000 (sawa na 60,236,000/- za madafu) kwa onesho hilo la masa mawwili katiika ukumbi wa klabu ndogo ya usiku ya Timepiece, alikaa kwenye hoteli hiyo kwa bei ya pauni 70 (sawa na 191,660/- za madafyu) kwa usiku mmoja.
Meneja wa hoteli hiyo, Debbie Hamnett, alisema Snoop na bendi yake walifanya booking toka July ila hakuna aliyejua ni yeye na kundi lake hadi walipofika na kuingia vyumbani.
Yeye na mwenye klabu kulikofanyika onesho hilo hadi sasa hawaamini kwamba alikuwa ni yeye.
Inasemekana Snoop Dogg alikuwa amepata tenda zinazolipa maradufu kufanya maonesho sehemu zingine ila akachagua hapo Exeter ambako mmiliki wa klabu ya Timepiece George Sloane alisikika akisema “Walipokubali kuja kufanya onesho nilidhani aidha anatania ama ametucahngaya sisi na klabu ingine ya usiku. Lakini Snoop Dogg na timu yake walikuwa wameshafanya utafiti kuhusu klabu hiyo na kugundua kuwa awali lilikuwa kanisa kuukuu, na baada ya kuona picha zake, walijua ni klabu ndogo ya usiku na kuamua kufanya onesho lisilokuwa na watu wa vurugu”
Rapa Snoop Dogg akiwa katika onesho katika kumbi wa klabu ndogo ya usiku ya Timepiece, Exter Uingereza
Hoteli aliyofikia Snoop Dogg na kuacha gumzo
Snoop Dogg akipata taswira na wafanyakazi wa hoteli hiyo
Chumba alicholala Snoop Dogg kwa bei ya takriban shilingi laki mbili kwa siku. Kutokana na utajiri alionao na dau la zaidi ya shilingi milioni 60 alizolipwa kwa onesho lake, gumzo limeachwa huko Exeter
Alafu wasanii wetu wanadanganya umma wanalipa watengenezaji movie wakienda UK Kama Tzsh million 30 wakati Snoop dog Hiyo show moja kalipwa million 60 karibu za Tanzania sasa hapo wangesema wasanii wetu wanalipwa karibia na Snoop Dogg Mapato.
ReplyDeleteSasa hiyo hotel ina ubaya gani?
ReplyDeleteDu hicho ndio chumba cha hali ya chini hadi kuwa gumzo? Kweli wengine tunasindikiza wenzetu hapa duniani?
ReplyDeleteNdio ni chumba cha hali ya chini kwa UK
ReplyDelete