FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama
“Safari National Pool Competition 2014”, mikoa ya Tabora ,Kagera,
Arusha,Kilimanjaro na Mkoa wa kimichezo wa Ilala zimefanikiwa kupata
mabingwa wa mikoa zilizomalizika mwishoni mwa wiki katika mikoa
hiyo.
Mkoa wa Tabora mabingwa ni Tiptop Pool Klabu,Kagera ni Bilele Pool
Klabu,Arusha ni Ngarenaro Pool Klabu,Kilimanjaro ni Mboya Pool Klabu
na Mkoa wa Kimichezo wa Ilala ni Mashujaa Pool Klabu ambavyo kwa
kutwaa ubingwa huo walizawadiwa pesa taslimu kila klabu Shilingi
800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za
kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Tabora ni Omary
Hassan, Kagera ni Roberth Butasigwa, Arusha ni Richard Daudi,
Kilimanjaro ni Baraka Jackson na Ilala ni Yasin Athuman ambao
walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa
yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa
Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake, Tabora ni Happiness
Morgan, Kagera ni Sajida Saidi, Arusha ni Merry Gumbo, Kilimanjaro
ni Reticia Kileo, na Ilala ni Recho Kihupi ambao walizawadiwa fedha
taslimu Shilingi 300,000/=.
Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion”
zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa
kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma.
Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka
huu mkoa wa Kilimanjaro.
Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba(kulia) akimkabidhi nahodha wa klabu ya Mashujaa, Said Miraji(Babu Jee) pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya uibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Wachezaji wa timu ya klabu ya Mashujaa wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi 800,000/= /= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba na Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...