![]() |
Bw. Ally Nchahaga - mratibu wa AutoFest. kushoto Erick Babu - Director wa DriveShaft magazine , kulia Bi. Mamou Ismail - Muakilishi wa Vision Investments wakati wa mkutano na wanahabari |
Likirudi kwa mwaka wake wa saba, tamasha la
magari Tanzania (autofest) litakua likionyesha magari mapya, matoleo mapya ya
pikipiki, burudani za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa nchini na
burudani nyingine za kusisimua kwa ajili ya familia nzima kuanzia Septemba
19-21, 2014. Tamasha la mwaka huu ambalo linaandaliwa na Vision Investment,
litafanyika katika viwanja vya Biafra, Kinondoni. Anayetarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika ufunguzi ni Mhe. Dk Abdallah O. Kigoda,
Waziri wa viwanda na Biashara.
‘’Tukio hili linahusisha moja ya maonyesho muhimu sana na yenye
mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto”. Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi
Mtendaji wa Vision Investments. “Lengo letu ni kuendelea kuleta aina mbalimbali
ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye ‘Autofest’ ili wadau wapate
kufurahia na kuridhishwa navyo.” alisema.
Tukio hili la mwisho wa wiki linategemea kuvutia zaidi ya
watu nusu milioni, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari
Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, Autofest sasa imekua ni Tamasha
muhimu katika ulimwengu wa vyombo vya moto, likiwa ni onyesho pekee
linalowaleta wapenzi wa magari pamoja. Ni onyesho kubwa linaloonesha magari ya
abiria, magari ya biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine
na zana zinazohusiana na magari.
Burudani kwenye tukio zitahusisha, ‘Bumper
to Bumper Auto Style Zone’ ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha
walivyoyapamba magari yao, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa
umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari
na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha
magari kama kubadilisha gia, kufunga breki, na kuselelesha gari.
“Mwaka huu tunatarajia kwamba matokeo
yatakua makubwa zaidi ukilinganisha na mwaka uliopita kutokana na kuongezeka
kwa matangazo na mahusiano ya umma,” alisema Nchahaga. “Autofest itapelekea
kutambulika kwa wadhamini wetu na program.” alisema.
Tamasha la Autofest linatoa nafasi za udhamini na maonesho.
Kampuni ya Vision Investment inakaribisha wadhamini na watu wanaotaka kushiriki
katika maonyesho ya mwaka huu kwa kujaza fomu ya maombi iliyopo katika mtandao
wa www.autofest.co.tz. Fulana za Autofest sasa zinapatikana kwa mauzo, na
mapato yatayopatikana yatatumika katika kuendeleza program za Autofest
Kuhusu Vision Investments
Vision Investments ni moja ya
sehemu ambapo mawazo ya mikakati mbalimbali na teknolojia mpya inapohitajika
ili kuweka biashara katika mstari wa mbele. Malengo ya Vision ni kutambua,
kuunda, kuendeleza, kutoa na kuuza masuluhisho yanayofaa kukidhi mahitaji ya
mteja ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu, uwezo na thamani. Vision pia ni
wataalamu wa mtandao,graphic design, ushauri wa Masoko na usimamizi wa matukio.
Kwa taarifa zaidi, tembelea: www.vision.co.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...