Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza (Mb) akifanya mazungumzo na Mhe. Jenerari James Wani Igga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini ofini kwake .

Na Bashiri Kalum 

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng Christopher Kajoro Chiza,( MB), amesema Tanzania ipo tayari kuendesha mafunzo ya kilimo katika vyuo vyake vya kilimo kwa wananchi wa Sudani, kuanzia ngazi ya cheti hadi ngazi ya shahada na kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na Sudani Kusini, kwa lengo la kukuza taaluma ya kilimo na  soko la mazao ya wakulima.
Mhe. Eng Christopher aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini sudani ya kusini ambapo alikutana na Mhe. Jenerali James Wani Igga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini ofisini kwake mjini Juba. 

Aidha waziri amezitaka wizara ya kilimo ya sudani kusini kushirikiana na wizara ya kilimo chakula na ushirika ya Tanzania ili kuimarisha  sekta hii kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwenye masokio ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wakulima kutumia zana bora za kilimo.

‘Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini inajukumu la kuimarisha uwekezaji katika kilimo ili wakulima wa nchi hizi mbili kuondokana na kilimo cha kujikimu na kuwa na kilimo cha kibiashara, ukizingatia kuwa fursa za kuleta mabadiliko hayo   zipo, hususan  ardhi inayofaa Kilimo, maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, hali nzuri ya hewa, huduma bora za ugani na pembejeo’ .alisema Chiza

Aidha katika ziara hiyo Waziri Chiza alitoa ahadi ya msaada wa kibinadamu wa  tani 500 za nafaka,uliototewa kwa ajili ya wananchi wanaoathirika na vita vya waasi katika baadhi ya majimbo  ya nchi hiyo.

Naye Jenerali James Wani Igga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini alifafanua kuwa, nchi ya Sudani ya Kusini asilimia 54 ya ardhi yake inafaa kwa kilimo, inyolimwa ni asilimia 4 tu, hivyo alitoa mwito kwa watanzania kwenda Sudani Kusini kuwekeza katika kilimo na usindikaji kwa lengo la kuongeza thamani mazao. Alisisitiza kuwa fursa nzuri za kilimo zilizopo ni uwepo wa ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo, mto Nile wenye maji mengi sana kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, Hali nzuri ya mvua kwa kipindi kirefu. 

Serikali ya Sudani ya Kusini imeiomba Tanzania  kusaidia kujenge  uwezo katika Ushirika, Utafiti, Mafunzo kwa maafisa ugani, na mengine mengi kama yatavyoanishwa katika andiko la ushirikiano  linalotayarishwa na wataalamu wa nchi hizi mbili.

Kwa upande wa wafanyabiashara  aliofuatana nao Mhe, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, wameishukuru serikali yao kwa kuwa karibu nao na kufanikiwa kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Jamhuri ya Sudani  Kusini. Aidha serikali ya Sudani Kusini  imeahidi kusimamia usalama wa wafanyabiashara kutoka Tanzania na mali yao na kuhakikisha kuwa biashara hiyo inafanyika .  

Serikali ya Sudani ya Kusini imeiomba Tanzania  kusaidia kujenga  uwezo katika Ushirika, Utafiti, Mafunzo kwa maafisa ugani, na mengine mengi kama yatavyoanishwa katika andiko la ushirikiano  linalotayarishwa na wataalamu wa nchi hizi mbili.

Kwa upande wa wafanyabiashara  aliofuatana nao Mhe, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, wameishukuru serikali yao kwa kuwa karibu nao na kufanikiwa kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Jamhuri ya Sudani  Kusini. Aidha serikali ya Sudani Kusini  imeahidi kusimamia usalama wa wafanyabiashara kutoka Tanzania na mali yao na kuhakikisha kuwa biashara hiyo inafanyika bila dhuruma.  

Mhe. Eng  Christopher  Kajoro Chiza katika ziara yake alifuatana na Mhe. Batilda Salha Burian Balozi wa Tanzania nchini Kenya,  Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, na wafanyabiasha wa mazao watano. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ...hapa nakumbuka ile hadithi ya kipofu kumuongoza kipofu njia. Wasipotumbukia shimoni wote ni majaliwa!!

    ReplyDelete
  2. Tanzania yenyewe inahitaji mafunzo sasa itamfundishaje mwenzake. Nawashauri wenzetu Wasudani wakajifunze kwa waliofanyikiwa kwatika kilimo.

    ReplyDelete
  3. yaani hiyo ni kama ile ambapo serikali iliamua watu walio maliza darasa la saba wawe walimu wafundishe wenzao shule ya msingi, vichekesho.tukawaita UPE yaani ualimu pasipo elimu, ndo hii ya Tanzania kufundisha kilimo Sudani, wao wenyewe kulima kwenyewe hawajui, wafundishe kulima inaingia akilini hii kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...