Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi (kulia),akimtwisha ndoo ya maji Radhia Said baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji mwishoni mwa wiki kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisika cha maji kiolichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 29  kwa msaada wa TBL katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Wanaopiga makofi ni wananchi wa eneo hilo wakionekana kufurahishwa na msaada huo muhimu kwani wataondokana na tatizo la maji ambapo walikuwa wakitembea zaidi ya KM 2 kununua maji ndoo moja sh. 700. Katika Kisima hicho watakuwa wananunua ndoo moja ya maji kwa sh. 50.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus, akifungua maji kwenye bomba lililounganishwa kwenye kisima hicho. Kisima hicho kina uwezo wa  kutoa zaidi ya lita 5000 za maji kwa saa.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana. Saidieni pia kufunga taa za mitaani ili kupunguza wizi na uhalifu. Taa hizo huitwa mulika mwizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...