FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari
National Pool Competition 2014”, mkoa wa kimichezo wa Temeke jijini
Dar es Saalaam na Dodoma zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa
mwishoni mwa wiki.
Mkoa wa kimichezo wa Temeke mabingwa ni klabu ya Mpo Afrika
walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa mwaka jana wakati mkoani
Dodoma Klabu ya Delux ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo.
Klabu ya Mpo Afrika na Delux kwa kutwaa ubingwa huo zilizawadiwa
pesa taslimu Shilingi 800,000/= kila klabu pamoja na tiketi ya
kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika
Mkoani Kilimanjaro.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Temeke; Innocent
Sammy alifanikiwa kutwaa ubingwa na Dodoma ni Rgnald Kassimu,
ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika
mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za
kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja mmoja Wanaume.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake,Temeke; Rebeca
Magaigwa alitwaa ubingwa na Dodoma ni Rehema Mussa, ambao
walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa
mchezaji mmoja mmoja upande wa Wanawake.
Wiki hii fainali za Safari Pool Competition 2014,ngazi ya mikoa
zinatarajiwa kuhitimishwa na mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya.
Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool
Competion” zinatarajiwa kufanyika Septemba 14
mwaka huu, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha
Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma
Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan
i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka
huu mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia)
akimkabidhi kikombe nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool
ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa
wa fainali za mchezo huo ujulikanao kama “Safari National Pool
Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika
Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa
Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis
Rungu.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia)
akimkabidhi pesa taslimu Shilingi 800,000/= nahodha wa timu ya klabu
ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya
kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari
National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke
uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni
Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya
Taifa, Denis Rungu.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wa klabu ya Mpo Afrika na mashabiki
wakishangilia na kikombe mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za
mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014”
ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...