Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Shule ya msingi Wamato (hawapi pichani) wakati walipowatembelea. |
100.5 Times Fm kwa kushirikiana na makampuni ya MeTL, Shamo, Simba Trailer, Hugo Domingo, M2
Advertising, Ifatar, kampuni ya vipodozi ya Darling walijitolea na kupata chakula cha jioni kwa watoto
wanaoishi katika mazingira magumu wanaosomeshwa katika shule ya msingi Wamato kwa
udhamini wa taasisi ya Help2Kids.
Tukio hilo lililofanyika wiki iliyopita liliambatana na michezo mbalimbali na hotuba zilizolenga katika
mipango ya kuisaidia zaidi shule hiyo ya msingi ya Wamato iliyoko eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam ili
kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora zaidi kwa maisha ya baadae.
Akiongea na 100.5 Times Fm, mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Basila Chuwa ameishukuru taasisi ya
Help2Kids kwa kuendelea kuisaidia shule hiyo kwa kila hali pamoja na makampuni yote yaliyojitokeza
kuhakikisha yanakuwa karibu na kituo hicho kwa lengo la kusaidia huku akitoa wito kwa makampuni
mengi zaidi kuiga mfano huo kwa kuwa serikali imelemewa.
Mwanzilishi wa Kituo cha MAWATO,Bi. Basila Chuwa |
“Nilikuwa na shirika la wa Canada lilikuwa linaitwa Canadian Christian Child Fund, ile ilinisaidia kwa
miaka zaidi ya kumi. Walikuwa wanafanya vitu vingi sana. Walijenga hata majengo haya, walikuwa
wanasaidia nguo, walikuwa wanawaangalia hata nyumbani wazazi. Hata sabuni ya kufulia walikuwa
wanawapatia na chakula. Lakini sasa hivi...serikali haiwezi kutusaidia kila kitu (serikali yenyewe
imelemewa).”
Ameeleza kuwa nia yake ni kuanzia ‘daycare’ sehemu ambayo watoto watakuwa wanaachwa kwa siku
nzima wakisoma na kuangaliwa huku wazazi wao wakiwa katika mihangaiko kisha wanawapitia jioni
wakielekea majumnbani. Lakini upungufu wa majengo ni moja kati ya kikwazo kikubwa.
Amesema mpango huo wa ‘daycare’ ni bora zaidi ya kuwa na kituo cha kuwatunza moja kwa moja
watoto kwa kuwa kufanya hivyo kutaendelea kuwaweka karibu na malezi ya familia na malezi ya kituo
pia.
Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa akizungumza jambo na baadhi ya watoto hao. |
Naye Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa amesema Times Fm inaendelea kutoa misaada
katika jamii na inakuwa sio tu sehemu ya jamii bali sehemu ya msaada pia kadri inavyowezekana na
kwamba kwa kipindi hiki wameamua kusaidia pia katika upande wa elimu kwa watoto ili kutengeneza
viongozi bora wa baadae.
“Times Fm ni radio ambayo inapenda kujishughulisha na shughuli za kijamii katika kusaidia jamii na
kama tunavyosema kwamba tusisubiri wafadhili, serikali ama taasisi ije kutusaidia. Kwa sisi wenyewe
tunaona kile kidogo tulichonacho tunajaribu kukaa na wadau tunatengeneza mipango tunakuja
tunafanya vitu kama hivi vya kusaidia watoto au communities mbalimbali.” Amesema Rehule Nyaulawa.
Amesema shirika la M2 Advertising liliguswa na shughuli za awali za kijamii zilizokuwa zikifanywa na
Times Fm awali kama kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kupaka rangi na kutoa vifaa kwa
kituo cha polisi cha Kawe, hivyo shirika hilo kaamua kuungana na mazoezi hayo ya kimaendelea na
kuyavuta makampuni mengine pia.
Bwana Rehure ameyashukuru makampunii yote yaliyoshirikiana na 100.5 Times Fm na kuendelea kutoa
wito kwa makampuni mengi zaidi kuungana na kituo hicho cha radio.
“Hili tulilifanya kama lilivyo na nafikiri ni njia nzuri ya kuanzia au kuwafuata na kuwaambia ‘jamani
tulifanya moja basi twendeni kwenye lingine na lingine’, na pia mashirika mengine ambayo yanahisi
kwamba yanaweza kufanya basi nayakaribisha.”
Kupitia mtandao wa Twitter, shirika la Help2Kids lilitoa shukurani zake kwa makampuni yote yaliyosaidia
katika kukamilisha tukio hilo.
“help2kids would like 2 say thank u 2 @M2Advertising & @TimesFMTZ 4 such a wonderful event
yesterday. U truly warmed a lot of child's hearts” Walitweet Help2Kids.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...