Afisa Vijana wa UMATI kutoka Temeke Bibi. Upendo Daud akimkabidhi
zawadi ya machapisho kuhusu Afya ya uzazi wa mpango Mwenyekiti wa Mtaa wa
Sabasaba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana lililofanyika
katika mtaa wake. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI
kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana
limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”.jpg)
.jpg)
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sabasaba wakipata maelezo kuhusu afya ya uzazi wa mpango kutoka kwa waelimisha rika wa UMATI walipokuwa katika Jamvi la Vijana lilioshirikisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.
Mmoja wa washereheshaji katika Jamvi la Vijana akimkabidhi mtoto Shani
Rajab zawadi ya Jarida la Fema baada ya kujibu swali kuhusu uzazi wa mpango
katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wa Sabasaba na kuhusisha Kikundi
cha Vijana cha Benki Club kutoka kata ya Mtoni iliyopo Manispaa ya Temeke
jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni. Jamvi la Vijana ni program ambayo
inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya
Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya
uzazi wa mpango?”
Baadhi ya wananchi wakifuatilia igizo kutoka kwa Kikundi cha Vijana
cha Benki Club (hakipo pichani) wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema
hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa ya
Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na
UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo
la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya waigizaji wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakiigiza
kuhusu namna ambavyo mwanaume anamshinikiza mke wake abebe mimba
mara baada ya miezi michache tokea ajifungue,igizo hilo lilionyeshwa wakati wa
Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba kata
ya Mtoni iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni
program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka
Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana
haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni
Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Bw. Ibrahim Mwita (waliosimama
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kikundi cha Vijana cha
Benki Club wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam mapema
hivi karibuni.
Picha zote na Frank Shija, MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...