Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu
Kayandabila akionyesha mbegu za mahindi zilizohifadhiwa kwenye ghala aina ya
Silo, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka
baada ya kuvunwa. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu
Kayandabila akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka
baada ya kuvunwa.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
Mmoja wa wadau wa kilimo akichangia mada katika uzinduzi wa jukwaa la kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa.
Ghala la kuhifadhia chakula aina ya Silo.
SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo, Chakula na
Ushirika imekili uwepo wa tatizo la upotevu wa mazao hasa jamii ya Mikunde na Nafaka
ambalo ni tatizo kubwa, linalowakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la wadau
watakaoangalia mazao mara baada ya kuvunwa jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Yamungu Kayandabila alisema, hata wizara yake inalitambua suala hilo, na
imeanza harakati za kupambana na janga hilo, hasa kwa kuwaamasisha wakulima na
wauzaji kutunza mazao hayo katika maghara.
“Tatizo la upotevu wa mazao ni tatizo kubwa, na
hilo linachangiwa na uhifadhi duni ambapo zaidi ya asilimia 30 utokea katika
upotevu wa mazao hayo,”alisema Kayandabila.
Kayandabila ambaye alikuwa mgeni rasm katika
uzinduzi wa jukwaa hilo ulioandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Ansaf,
aliipongeza taasisi hiyo kwa jitihada ambazo wanazionyesha katika kukomesha
tatizo hilo, huku pia akiyataka mashirika, taasisi mbalimbali kuiga mfano wa
Ansaf.
“Tunawashukuru sana Ansaf kwa kufanya uzinduzi
huu, na naimani taasisi na mashirika mengine yatafuata nyayo zao katika
kutokomeza suala hili la upotevu ili wakulima na wafanya biashara waweze
kuzihifadhi vizuri,”alisema Kuyandabila na kusema kuwa Serikali pekee haiwezi
bila ya sapoti ya watu kama wao.
Naye Katibu Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge
alisema, wamegundua changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba
wakulima na wafanya biashara kwa ujumla na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya
kuzindua jukwaa hilo.
Naye mmoja wa wajumbe walioudhulia uzinduzi huo,
Lusekelo Mwandemange ambaye ni mkulima wa zao la Mpunga kutoka Kyera, alisema,
amefarijika kupata nafasi hiyo, huku akiwataka Ansaf kuhakikisha wanatoa elimu
zaidi kwa wakulima walioko Mikoa mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...